EU kupambana na mashambulio ya kigaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mawaziri wa umoja wa ulaya

Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jumuia ya Umoja wa Ulaya wamekubaliana kushirikiana kwa ukaribu zaidi na serikali za nchi za kiarabu pamoja na nchi nyingine duniani kuzuia mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa kiislamu, kufuatia shambulio baya la mauaji lililotokea katika mji mkuu wa Ufaransa Paris, mapema, mwezi huu.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema mawaziri waliokutana mjini Brussels kwa mara ya kwanza wameonesha kutambua umuhimu na kuhitaji kufanya kazi pamoja.

Amesema Umoja wa Ulaya unakusudia kuzinduz mradi wa pamoja wa kupambana na ugaidi na nchi nyingine nyingi na pia kuweka Waambata wa usalama kati ya wawakilishi wa Umoja wa Ulaya.