BBC kumuenzi Komla Dumor .

Haki miliki ya picha
Image caption Komla Dumor

BBC imeanzisha tuzo za kumuenzi na kwa heshima ya aliyekuwa mtangazaji wake Komla Dumor,mwaka mmoja baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka arobaini na mmoja.

Komla Dumor alikuwa ni mtangazaji wa kipekee aliyekuwa na kipaji cha tofauti mwenye asili ya Ghana,na katika kipindi kifupi cha uhai wake alifanya kazi ya kutukuka na kuacha athari zake Afrika na dunia kwa ujumla.

Tuzo hiyo endapo atapatikana mshindi,basi itakwenda kwa mtu anayefanya kazi na kuishi barani Afrika,ambaye anauzoefu mkubwa katika kazi ya uandishi wa habari,na uwezo wa kipekee wa kuwasilisha habari kutoka barani Afrika.

Na mshindi wa kinyang'anyiro hiki atajishindia muda wa miezi mitatu kufanya kazi na BBC mjini London.