Usugu wa vimelea vya Malaria kutafitiwa

Image caption Mbu

wanasayansi wanatafiti namna vimelea vya ugonjwa wa malaria jinsi vinavyoendelea kuwa sugu kwa dawa zilizokuwa zinatibu ugonjwa huo ili kugundua kinachosababisha dawa hizo kukosa nguvu ya kutibu.

Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la kitabibu la journal Nature Genetics,watafiti hao wanasema kwamba ,mwaka 1950, dawa baada ya dawa zilishindwa kupambana na vimelea vya malaria.

Kwa mara ya kwanza utafiti huo uligundua vimelea vya ugonjwa malaria katika mpaka wa Thai Cambodia,kabla ugonjwa huo haujasambaa barani Afrika na kwingineko ulimwenguni.

Kwa sasa wanasayansi hao wamegundua dawa ambayo vimelea vya ugonjwa huo havina ujanja wa kukwepa kutokomezwa.na kuna imani kwamba katika tafiti kadhaa zijazo huenda mwanga ukapatikana na kugundua sababu za vimelea hivyo kuzidi kuwa na nguvu ya usugu .