Mume akiri kumchinja mkewe London

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Naveen Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa kwa mauaji tarehe 28 Januari

Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini London.

Naveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.

Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.

Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tahira Ahmed alipatikana akiwa amechinjwa nyumbani kwao mjini London

Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.

Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.

Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.