Kwa nini mtu achorwe Tatoo machoni?

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kufungwa jela kwa mhalifu mwenye tatoo kwenye jicho lake mjini Alaska kumezua gumzo sana nchini Marekani kuhusu hatua wanazochukua waru kurembesga nyuso zao.

Bila shaka hili pia limezua gumzo kwani ni kasumba ambayo ndio imeanza kuchipuka na kuwavutia watu wengi sna.

Jason Barnum, mwenye umri wa miaka 39, ambaye alikiri kosa la kujaribu kumuua afisa wa polisi, ana tattoo ndani ya jicho lake kwenye paja la uso, katika sehemu ya uso wake, kwenye meno yake na katika shavu lake.

Lakini cha kuvutia zaidi ni kuwa sehemu nyeupe ya jicho lake imewekwa tatoo kwa kutumia wino mweusi.

Upande wa mashitaka ulisema kwamba mtuhumiwa kwa kuangalia tu uso wake uliojaa tatoo, ni ishara kwamba ni uamuzi alioufanya kitambo sana,uamuzi wa kuwa mhalifu.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Baadhi wanapenda macho yao kuwa na mweonekanao wa rangi nzuri ya kupendeza

Lakini je kwa kuweka tatoo ndani ya macho yake, alitaka kuonyesha kwamba ni mhalifu na mpenda vurugu?

Mwanamume wa kwanza aliyejaribu kujidunga wino kwenye macho yake alikuwa mtaalamu na mchoraji wa Tatoo, anayejulikana kama Luna Cobra.

Hakuwa na nia ya kufanana na mtu muovu bali lengo lake lilikuwa kufanana na viumbe vilivyokuwa kwenye filamu maarufu ya Dune.

''Wakati unapodungwa ile sindano inayoweka wino kwenye macho yako unahisi kama mtu anakudunga kisha unahisi kama mtu umewekewa mchanga ndani ya macho,'' anasema Cobra ambaye kazi yake sasa ni kurembesha watu macho na kuwabadilisha rangi za wacho yao. Anaishi nchini Canada.

Sindano moja huwa na wino wa kutosha kufunika robo ya jicho. Unahitaji zaidi ya sindano moja ya wino kubadilisha rangi ya sehemu nyupe ya jicho. Rangi hio huwa ni ya kudumu haiwezi kutoka tena.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kylie anasema watu wamepnda sana rangi ya macho yake

Kylie Garth

Kylie ana macho ya buluu na anasema kwamba watu wengi humtizama sana kitu anachokifurahia.

Kylie anafurahishwa sana kuwa na mwonekanao wa kipekee ikizingatiwa kwamba yeye hufanya kazi katika duka ambalo hutoa huduma kwa wanaotaka kutogwa mjini Sydney Australia.

Kabla ya kuamua rangi ya wino aliotaka kutumia ndani ya macho yake, Garth aliwahi kujaribu kuweka tatoo mbali mbali ikiwemo kwenye uso wake, kutoga masikio yake na hata ulimi wake.

Jason Barnum anasema unapobadilishwa rangi ya mambo, unahisi kama mtu anakudunga kisha unahisi shinikizo flani halafu unahisi kama umemwagiwa mchanga kwenye jicho lakini hauhisi uchungu wowote. ''

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanamuziki huyu alisema alihisi macho yake yalikuwa yanachomeka baada ya kufanyiwa tatoo ya jicho

Hata hivyo mwanamuziki mmoja wa Poland anatofautiana na wanavyosema wengine. Alinaswa kwenye kanda ya video akiwekwa tatoo ndani ya jicho lake. Siku chache baadaye, alihisi kama vile jicho lake linachomeka hali iliyomzuia hata kulala.

Garth anasema kwamba macho yake yamewapendezea wengi sana.

Labda ni lile wazo tu la mtu kudungwa sindano ndani ya jicho lake ndilo linawahofisha wengi. Watu huniambia, ''eeh, siamini ulifanywa hivyo. Lakini sijawahi kusikia mtu akisema kwamba ninatisha.''

Luna Cobra hata hivyo anasema yeye huwashauri vijana kusubiri hadi wapate kazi kabla ya kuanza kujibadilisha rangi ya macho, kwa sababu huenda ikawakosesha kazi. Kile alichoanza kukifanya kama jaribio la kujifurahisha tu kwa kutaka kuwa na mwonekano wake wa kikepekee kimewavutia watu wengi sana.

Lakini madaktari wa macho walanaani kasumba hii wakisema ni hatari na inaweza hata kumfanya mtu kupofuka.