Papa Francis azungumzia familia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani ameunga mkono haki ya wazazi kuchagua ukubwa wa familia zao.

Amesema waumini wazuri wa Kanisa katoliki hawapaswi kuzaa bila ya mpangilio.

Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani amelalamikia mawazo ya nchi za magharibi kuhusu kudhibiti uzazi na haki za wapenzi wa jinsia moja kuwa yamezidi kushinikizwa katika familia za nchi zinazoendelea.

Wakati wa ziara yake, Papa Francis ametetea utamaduni wa mafundisho ya kanisa katoliki unaopinga matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.

Wakati wa ziara yake nchini Ufilipino, inakadiriwa kuwa watu milioni sita walihudhuria ibada iliyoendeshwa na kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani, katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manila.