Vinu vya mafuta kupunguza wafanyakazi

Image caption Kinu cha utafutaji mafuta

Moja ya kampuni kubwa za mafuta Talisman Sinopec imetangaza mpango wake wa kupunguza wafanyakazi wake wapatao mia tatu kutoka katika sehemu ya pwani ya uzalishaji .

Kampuni hiyo ya Talisman imeanisha kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo watao 100 na na wakandarasi 200 wataathiriwa na mpango huo na hivyo kufanya idadi ya waathirika kufikia mia tatu.

Kampuni hiyo imeendelea kufafanua kwamba imelazimika kuchukua hatua hiyo ili kukabiliana na kushuka kwa bei ya mafuta ulimwenguni na kwa upande wao, ili waweze kupata nafuu katika gharama za uendeshaji.

Vilio vya wafanayakazi kupunguzwa kazi ili kukabiliana na gharama za uzalishaji havitaishia kwenye kampuni hiyo ya Talisman tu lah hasha, kwani mpango kama huo wa kupunguza wafanyakazi umeshatangazwa hivi karibuni na makampuni ya BP, Shell, Chevron na Conoco Phillips .

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Talisman Sinopec bwana Paul Warwick amesema kwamba kampuni yake inafanya kazi katika mazingira thabiti kinyume na kuanguka kwa bei ya mafuta ulimwenguni na haijaongeza gharama za uzalishaji pamoja na kuanguka kwa uzalishaji pia kuna gharama za uzalishaji,utafutaji mafuta,na masuala ya ukarabati mitambo vyote vinawakabili .

Hatuna kitu chochote kitakachozuia changamoto hiyo lakini tunachukua hatua stahiki za kukabiliana nazo.Tumekwisha ongea na nguvu kazi yetu, wametuelewa na wanatuunga mkono katika hatua tunazotarajia kuzichukua.