Mwanajeshi wa UK hatiani kwa kumbaka mtoto

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ikiwa atapatikana na hatia mwanajeshi huyo atafungwa jela miaka 10

Mwanajeshi mwingereza ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka na kumdhalilisha mtoto mwenye umri wa miaka 6 nchini Austria.

Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mwanajeshi huyo ambaye hajatajwa alikamatwa mwezi Novemba katika eneo la Tyrol ambako alikuwa anafanya mazoezi yake ya kijeshi.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 10 mwezi Machi.

Msemaji wa kiongozi wa mashtaka alisema kua wendeshja mashtaka wanaamini kwamba mwanajeshi huyo aliingia nyumbani kwa familia ya msichana huyo akiwa mlevi nyakati za asubuhi na kufanya kitendo hicho.

Mwanajeshi huyo alipatikana katika chumba cha mtoto huyo baada ya babake kusikia kelele.

Alikamatwa mjini Neustift na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka 10.

Msemaji wa kiongozi wa mashtaka aliambia BBC kuwa mtoto huyo alihojiwa na kiongozi wa mashitaka.