Bangi halali kwa matibabu Jamaica

Image caption Mswada wa kuhalalisha uvutaji wa Bangi utaidhinshwa na baraza la Senate wiki ijayo

Baraza la mawaziri la Jamaica, limeidhinisha mswada ambao unahalalisha watu kumiliki kiwango kidogo cha Marijuana.

Ina maana kwamba hii ni mara ya kwanza kwa jamii ya 'Warastafarian' wanaotumia Bangi kwa sababu za kidini kuweza kuivuta hadharani bila ya kupatikana na hatia.

Mswada huo,pia unatawezesha kuwepo halmashauri itakayokua ikitoa leseni za kupandwa , kuuzwa na kusambazwa kwa Marijuana kwa sababu za kimatibabu.

Lakini uvutaji wa Bangi katika maeneo ya umma haitaruhusiwa. Mswada huo huenda ukaidhinishwa na baraza la Senate wiki ijayo.