Kadi za kupigia kura, kikwazo Nigeria

Mshauri mkuu wa masuala ya usalama nchini Nigeria ameitaka tume ya uchaguzi nchini humo kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujayo ili kupata muda zaidi wa usamabazaji wa kadi za kupigia kura .

Mshauri huyo wa masuala ya usalama Sambo Dasuki, aliyasema hayo mjini London, amezielezea kadi za wapiga kura milioni 30 zilikwisha sambazwa tangu mwaka jana na idadi kama hiyo bado haijasambazwa .

Uchaguzi huu wa tarehe 14 February mwaka huu,ni mkubwa kuwahi kufanyika nchini Nigeria unaowataka wananchi wake kutumia kadi ya mpiga kura.Mpango huo unalenga kuzuia uibaji wa kura na kudanganya kwenye matokeo.

Raisi wan chi hiyo Goodluck Jonathan anagombea nafasi hiyo akichuana na mpinzani wake aliyewahi kuwa mtawala wa kijeshi Muhammadu Buhari.

Bwana Dasuki, amemwambia mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (Inec) kwamba itakuwa na maana sana endapo wata ahirisha uchaguzi huo kwa kipindi cha miezi mitatu ingawa wazo la kuahirisha uchaguzi huo tayari limekumabana na upinzai kutoka kwa msemaji wa upinzani nchini humo Lai Mohammed, huku akihoji kwanini serikali haiko tayari ,kwanini uchaguzi uahirishwe? Na kusema kuwa upinzani hauko tayari na hajafurahishwa na wazo hilo ,na kwamba haitawagharimu serikali chochote na uchaguzi huo ni halali kisheria.

Uchaguzi huo unapigwa wakati huu baada ya utawala wa muda mrefu wa kijeshi uliohitimishwa mwaka 1999.

Rais Jonathan anatoka katika chama cha PDP akichuana na Buhari ambaye aliiongoza Nigeria tangu mwaka 1984 hadi August mwaka 1985 baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Nigeria inataka kuingia kwenye uchaguzi ilhali kuna mapigano yanayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam la Boko Haram upande wa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.