Serikali ya Yemen hatimaye yajiuzulu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption waasi wa houthi wakiuzunguka mji mkuu wa yemen Sanaa

Mgogoro nchini Yemen umechukua mkondo mwengine alhamisi baada ya ripoti za maafisa kusema kuwa Rais na waziri mkuu pamoja na serikali yao wamejiuzulu.Hatua hiyo inajiri baada ya serikali hiyo kutoa ombi la kujiuzulu huku kukiwa na switofahamu kati yake na waasi wa Houthi maafisa wamesema.

Serikali hiyo ilibuniwa mnamo mwezi Novemba kufuatia makubaliano yalioafikiwa na umoja wa mataifa.

Wapiganaji wa Houthi bado wanaendelea kudhibiti mji mkuu wa sanaa mbali na kumteka msadizi mmoja wa rais wiki iliopita.

Walikuwa wamekubali kuondoka katika maeneo muhimu katika kasri ya ikulu ya rais na nyumba ya rais Abdrabbuh Mansour Hadi.