Wanawe Mubarak waachiliwa Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Alaa na Gamal Mubarak wameachiliwa nchini Misri

Wanawe wawili wa kiume aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak, wameondoka gerezani.

Mahakama iliamuru wawili hao Alaa na Gamal Mubarak, kuachiliwa huku kesi yao ya tuhuma za ifisadi dhidi yao ikisubiriwa kuanza upya.

Wawili hao walionekana kama wafisadi wakuu wakati wa utawala wa Mubarak huku maandamano yaliyomuondoa mamlakani Mubarak yakisemekana kuchochewa pakubwa na dhana kwamba Gamal alikuwa anatayarishwa kumrithi babake.

Mwaka jana walifungwa jela miaka minne pamoja na baba yao.

Mahakama wiki mbili zilizopita ilitupilia mbali uamuzi dhidi ya Mubarak na kusema kesi ya tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma dhidi yake itasikilizwa upya.