Chanjo ya ukimwi yaweza patikana

Melinda na Bill Gates Haki miliki ya picha bbc

Muasisi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates, anasema anaamini kuwa idadi ya watu wanaougua UKIMWI inaweza kupungua kwa zaidi ya 95% katika miaka 15 ijayo, iwapo chanjo na dawa za kutibu ugonjwa zitafanikiwa kutengenezwa.

Akizungumza katika Mkutano wa Uchumi wa Davos, Bill Gates alisema ana matumaini kuwa maendeleo hayo yataweza kupatikana ufikapo mwaka wa 2030.

Mfuko wa Bill na Melinda Gates umetumia mamilioni ya dola kugharimia utafiti kuhusu UKIMWI.