Liberia yakaribia kuangamiza Ebola

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ebola Liberia

Nchi ya Liberia ambayo iliathirika vibaya na ugonjwa wa ebola eneo la magharibi mwa Afrika inasema kuwa kwa sasa ina visa vitano tu vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo.

Naibu waziri wa afya Tolbert Nyenswah alisema kuwa Liberia iko karibu kuangamiza ugonjwa huo.

Hii ni ishara ya hivi punde kuwa ugonjwa huo ambao umewaua maelfu ya watu nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone unaangamizwa kufuatia msaada mkubwa wa kimataifa.