Waziri wa madini ajiuzulu Tanzania

Image caption Waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Sospeter Muhongo amejiuzulu

Waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu,na kumfanya kuwa afisa wa tatu wa ngazi za juu serikalini kuathiriwa na ufisadi uliokumba sekta ya kawi katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Professa Muhongo alitoa tanagazo hilo wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Kujiuzulu kwake kunajiri baada ya kufutwa kazi kwa waziri wa Ardhi na kujiuzulu kwa mwanasheria mkuu ,wote wakiwa wamehusishwa na kutolewa kwa zaidi ya dola milioni 120 kutoka kwa benki kuu ya taifa hilo kupitia mazingira ya kutatanisha.