Raia waandamana dhidi ya Houthi Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia waandamana kupinga kundi la wapiganaji wa Houthi mjini sanaa

Maelfu ya watu wameingia mitaani ya mji mkuu wa Yemen Sanaa katika maandamano ya kupinga waasi wa kishia wanaojulikana kama Houthi ambao wamedhibiti mji huo.

Waandamanaji hao wameripotiwa kuelekea katika kasri la rais Abdrabbuh Mansour Hadi kupinga kujiuzulu kwake siku ya alhamis.

Marekani inasema kuwa inaendelea kuwa na ushirikiano katika kapambana na ugaidi na Yemen laikini shirika la habari la Reuters linasema kuwa oparesheni nyingine za kupambana na kundi la al-Qaeda zimesitishwa.