DRC: kipengele cha utata chaondolewa

Maandamano ya KInshasa ya jula lilopita Haki miliki ya picha Reuters

Bunge la wawakilishi la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo limepitisha mswada uliorekibishwa kuhusu uchaguzi, baada ya kuondoa kipengee kilicholeta utata, na ambacho upinzani unasema kingerefusha awamu ya uongozi wa Rais Kabila.

Mswada ulivyopitishwa awali juma lilopita ulizusha maandamano ya siku kadha.

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema watu 40 walikufa katika maandamano hayo.

Mswada wa awali ulitaka kufanywe sensa kabla ya uchaguzi wa rais - upinzani uliona kuwa hiyo itachelewesha uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanywa mwaka ujao.