Sheria tete ya uchaguzi DRC kutupwa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption drc

Spika wa bunge nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo amesema kuwa mabadiliko yaliozua utata katika sheria ya uchaguzi nchini humo yatatupiliwa mbali.

Mabadiliko hayo yalitaka shughuli ya kuhesabu watu kufanyika kabla ya uchaguzi wa urais ambao utafanyika mwaka ujao.

Makundi ya upinzani yalisema kuwa lilikuwa ni jaribio la rais Joseph kabila la kutaka kubaki madarakani kwa kuwa katiba haimruhusu kugombea tena urais.

Baada ya mswada huo kudhinishwa na bunge, kulishuhudiwa maandamano ya siku tatu kwenye mji mkuu Kinshasa na maeneo ya mashariki mwa nchi ambapo wanaharakati wanasema kuwa zaidi ya watu 40 waliuawa.