Ebola ni funzo kubwa kwa WHO na dunia

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan Haki miliki ya picha AP

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, ameeleza mpango wa kuliimarisha shirika hilo baada ya malalamiko mengi kuhusu namna WHO ilivyoshughulikia mripuko wa Ebola Afrika Magharibi, ambayo imeuwa watu zaidi ya 8,000.

Margaret Chan alielezea mripuko huo kuwa maafa ambayo ni funzo kubwa kwa ulimwengu na WHO.

Katika kikao cha viongozi wa WHO mjini Geneva, Bibi Chan alisema mbinu za kupambana na misukosuko kama hiyo zinafaa kuimarishwa na kuanzishwe mfuko wa kugharimia hali ya dharura.

Alisema maafa ya Ebola yameonesha piya kwamba mfumo mwema wa afya wa taifa ni kitu cha lazima, siyo anasa.