Rais mpya wa Zambia aapishwa

Edgar Lungu wakati wa kampeni Haki miliki ya picha bbc

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu, ameapishwa baada ya kumshinda mwenzake kwa kura chache.

Bwana Lungu aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika sherehe hiyo kwenye uwanja wa michezo mjini Lusaka, kwamba yeye ni mtumishi wa watu.

Alipata asili-mia-48 ya kura, ikilinganishwa na asili-mia-47 za mgombea wa upinzani, Hakainde Hichilema.

Tume ya uchaguzi imekanusha malalamiko ya upinzani kwamba kumefanywa udanganyifu.