Kamanda wa LRA kupandishwa kizimbani ICC

Image caption Dominic Ogwen

Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Lord resistance Army,Dominic Ong'wen atafikishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the hague nchini uholanzi. atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Ong'wen ni kiongozi wa juu wakwanza kutoka katika kundi la waasi la Uganda, LRA kufikishwa mahakamani baada ya miongo miwili ya mapigano dhidi ya Serikali ya Uganda.

Mahakama ya ICC imesifu hatua hii ikisema kuwa ni hatua yenye kuelekea kumaliza visa vya kigaidi vinavyotekelezwa na LRA