Syriza yashinda uchaguzi,Ugiriki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alexis Tsipras,kiongozi wa chama cha Syriza

Chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza ambacho kimekuwa kikipinga hatua ya kubana matumizi kimeshinda katika uchaguzi uliofanyika nchini humo,japo kuwa hakuna uhakika kama kina viti vya kutosha Bungeni kuweza kuongoza serikali. Kiongozi wa chama cha Alexis Tsipras amewaambia wafuasi wake kaytakia mji mkuu Anthens kuwa hatua ya kubana matumizi iliyotangazwa na serikali inayoondoka imefikia mwisho na watafanya kazi na wakopeshaji na kukubaliana namna ya kushughulikia madeni ya taifa. Waziri mkuu anayeondoka madarakani Antonis Samaras amemtaka kiongozi wa chama cha Syriza Alexis Tsipras kumpongeza. Samaras anadai kuwa sera zake zilisaidia kufufua uchumi wa Ugiriki na kwamba walichukua hatua kudumisha hali ya usalama wa raia. Amesema kuwa anakabidhi nchi ambayo ni mwanachama wa umoja wa Ulaya na sarafu ya euro.