Ongwen afikishwa katika mahakama ya ICC

Image caption ongwen icc

Kiongozi mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen, amekuwa mwanachama wa kwanza wa kundi la Lord's Resistance Army LRA, kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake huko The Hague, Bwana Ongwen alithibitisha kuwa ndiye, huku akijieleza kuwa ni mwanajeshi wa zamani wa LRA.

Image caption Mahakama ya Icc

Anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa mengine ya kivita, ikiwemo mauwaji na utumwa.

Awali mwezi huu alikuwa amezuiliwa nchini Afrika ya kati, miaka kumi tangu ICC ilipotoa ilani ya kumkamata.