Daktari afungwa kwa ukeketaji Misri

Image caption FGM misri

Katika kesi cha kipekee nchini Misri, daktari mmoja ametiwa mbaroni kwa kosa la kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka kumi na tatu.

Wakereketwa wanaopinga tabia ya kuwakeketa watoto wa kike, walishtuka baada ya mahakama kumwachilia huru Daktari Raslan Fadl mwezi Novemba mwaka jana.

Lakini baada ya kesi kusikizwa upya, amehukumiwa zaidi ya miaka miwili gerezani.

Ingawa ukeketaji wa wasichana ulipigwa marufuku miaka sita iliyopita nchini Misri, zoezi hilo bado linaenea pakubwa.

Wale ambao wanajaribu kupambana na ukatili huo wameelezea hukumu ya Daktari Fadl kuwa ni ushindi mkubwa kwao.