Manusura wa Auschwitz waionya dunia

Image caption Kumbukumbu

Manusura wa mauaji ya kimbari katika kambo ya Auschwitz wameihimiza dunia kutoruhusu uhalifu wa mauaji hayo ya Holocaust kurudiwa tena wanapoadhimisha miaka 70 ya kukombolewa kwa kambi hiyo.

"sisi manusura hatutaki tuliyoyapitia yawe ndio mustakbala wa watoto wetu," alisema Roman Kent,aliyezaliwa mwaka 1929, alipohutubia waliohudhuria kumbukumbu katika kambi hiyo ya kifo nchini Poland.Takriban manusura 300 wa Auschwitz walirejea kwa ajili ya kumbukumbu hiyo chini ya hema kubwa.

Inakisiwa watu millioni 1 na laki 1,wengi wao wakiwa Wayahudi waliuwawa kati ya miaka ya 1940 na 1945 kambi hiyo ilipokombolewa na majeshi ya Sovieti.

"Kwa mara nyingine tena vijana wa Kiyahusi wanaogopa kuvaa vikofia vya " yarmulkes" katika mitaa ya Paris, Budapest, London na hata Berlin"

anasema Ronald S Lauder,Rais wa Jumuiya ya Wayahudi Duniani World Jewish Congress aliwaambia waliokusanyika "kwa mara nyingine tena Wayahudi wanalengwa barani Ulaya kwa sababu ni Wayahudi" .

Katika mji mkuu wa Czech , Prague, Spika wa mabunge ya nchi za Muungano wa Ulaya walikusanyika pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Wayahudi wa Ulaya na kutoa azimio la kulaani ubaguzi na uhalifu wa chuki dhidi ya Way