Liverpool kuvaana na Chelsea "Darajani"

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Anfield

Baada ya kushindwa kutambiana katika mchezo wa kwanza wa Kombe la FA uliomalizika kwa Sare ya 1-1 Chelsea na Liverpool watakuwa dimbani Stamford Bridge Jumanne kupimana ubavu.

Mchezo huu wa nusu fainali ya pili utaamua nani anaelekea fainali itakayopigwa katika dimba la Wembley Machi Mosi.

Katika mchezo wa kwanza Chelsea walipata goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Eden Hazard huku Raheem Sterling akiisawaizishia Liverpool.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya pili utapigwa kati ya Sheffield United na Tottenham.

Tottenham walipata ushindi katika mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 lilikwamishwa wavuni na Andros Townsend kwa mkwaju wa penati.