Mkutano kuhusu Faru weupe Kenya

Mkutano wa kimataifa utakaojadili jinsi ya kukabiliana na biashara haramu ya pembe za wanyama wanaokabiliwa na tishio kubwa la kuangamia unatarajiwa kuanza hii leo katika mbuga ya wanyama ya Ol Pajeta iliyoko kaskazini mwa kenya.

Wajumbe kutoka mataifa kadhaa duniani na wadau wote wa sekta ya utalii na wanyama pori nchini kenya wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao utaangazia jinsi ya kuhifadhi vifaru weupe ambao kwa mujibu wa takwimu za mwaka uliopita ni chini ya vifaru elfu tano kati ya hao kuna vifaru weupe chini ya watano waliosalia kote duniani ambapo wanne kati yao wapo nchini kenya.

Endapo juhudi hazitafanyika kuwahifadhi basi huenda wanyama hawa wakatoweka kabisa duniani chini ya miaka ishirini ijayo.