Urusi kuwekewa vikwazo zaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Urusi, Vladmir Putin

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Ulaya watakutana mjini Brussels kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kufuatia mashambulizi ya Mashariki mwa Ukraine.

Mkutano huu wa dharula umeitishwa baada ya raia 30 kuuawa kwa makombora, mauaji yaliyotekelezwa na Waasi wanaodaiwa waliungwa mkono na Urusi na kushambulia bandari ya Mariupol wikiendi iliyopita.

Majeshi ya NATO yamesema mamia ya vifaru vya Urusi, Magari ya Silaha yalikua Mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi imekana kujihusisha moja kwa moja na mashambulizi hayo.