Chad na Nigeria kuwakabili Boko Haram

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram

Serikali ya Chad imesema kuwa imewaondoa wapiganaji wa kundi la Boko Haram waliokuwa katika mji wa Malumfatori Kaskazini Mashariki mwa Nigeria,wameiarifu BBC viongozi wa juu wa Niger.

Majeshi ya Chad yamefanikiwa kuukomboa mji huo uliokuwa ukikaliwa na Boko Haram baada ya mapigano makali ya siku mbili ya anga na nchi kavu.

Taarifa kutoka nchini Niger zinasema kuwa vikosi vya wanajeshi wa ardhini wa Chad waliufikia mji huo kwa kukatisha ziwa Chad..

Wapiganaji hao wa Boko Haram wamewateka mamia ya watu na kuwapeleka kaskazini Mashariki mwa Nigeria eneo wanalolishikilia.

Serikali ya Nigeria imesema kuwa wanafanya kila kinachowezekana kuweza kuwadhibiti Boko Haram kwa kushirikiana na majirani zao Niger na Cameroon.

Chad tayari imetuma majeshi yake Cameroon kusaidia ambapo wiki iliyopita Nigeria ilitangaza kuwa majeshi ya Chad yatakuwa yakipigana katika ardhi yake.