Mpinzani wa Obama mwaka 2012 ajiondoa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mitt Romney aliyeshindwa na Obama uchaguzi wa 2012

Mitt Romney, mgombea wa chama cha Republican aliyeshindwa na rais Obama katika uchaguzi wa mwaka 2012 ameamua kutowania tena wadhfa huo.

Bwana Romney mwenye umri wa miaka 67 amesema kuwa ameamua ni muhimu kuwapatia viongozi wengine katika chama hicho fursa ya kuchaguliwa kama wagombea.

Taarifa yake inajiri wiki kadhaa baada ya tangazo lake kwamba atawania kwa mara nyengine.

Hatua yake ya kutowania inawapa fursa wafadhili kuwaunga mkono wagombea wengine.

Aliyekuwa Gavana wa jimbo la Florida Jeb Bush ,gavana wa new Jerzy Chris Christie na seneta Rand Paul ni miongoni mwa wale wanaowania kuingia ikulu ya whitehouse.