Ebola:Shule zaendelea kufungwa Liberia

Image caption Wanafunzi

Liberia imehairisha kufunguliwa kwa shule kote nchini kutokana na sababu kuwa hazijajiandaa kikamilifu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

Shule zilifungwa mwezi Julai mwaka uliopita katika jitihada za kukabiliana na janga hilo na zilipangiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu.

Mwandishi wa BBC nchini Liberia anasema kuwa shule kadhaa zilionekana kutojiandaa ili kuzuia maambukizi ya ungonjwa huo zikikumbwa na ukosefu wa maji ya kuosha mikono na vifaa vya kupima joto la mwili.

Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 3600 nchini Liberia lakini nchi hiyo kwa sasa ina visa vitano tu vilivyothibitishwa.