IS yamuua mateka mwengine wa Japan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kenji Goto

Japan imeelezea ghadhabu yake kwa kundi la wanamgambo la Islamic State ambalo limetoa kanda ya video inayoonyesha mauaji ya mateka raia wa nchi hiyo Kenji Goto.

Japan imeyataja mauaji hao kuwa kitendo cha kikatili ambapo waziri mkuu wa Japan mwenye hasira amesema kuwa japan itaendela kushirikiana na nchi zinazopambana na kundi hilo.

Wiki moja iliyopita mateka mwingine raia wa Japan Haruna Yukawa aliuawa na wanamgambo hao.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Familia ya Kenji Goto

Kanda ya video ya hivi punde inafanana na zile zilizokuwa zikionyesha kuuawa kwa mateka wengine awali.

Kenji Goto ambaye ni mwandishi wa habari alitekwa nyara nchini Syria mwezi Oktoba mwaka uliopita.