Jordan yalaani mauaji ya Mwandishi

Mfalme Abdullah wa Jordan ameyalaani mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Japan yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Ameyaita mauaji hayo ya Kenji Goto kuwa nitendo la kihalifu, uwoga na kuongeza kuwa juhudi zinafanywa kuweza kuachiwa huru kwa Rubani raia wa Jordan ambaye anashikiliwa na kundi hilo.

Maafisa wa usalama nchini Jordan wamesema wamekuwa wakijaribu kufahamu kama rubani huyo Muath al-Kasaesbeh yuko hai. Msemaji wa serikali amesema Jordan ilikuwa na nia ya kumuachia huru mwanachama wa al Qaeda, mlipuaji bomu Sajida al Rishawi, kama njia ya kubadilishana kuweza kuachiwa huru kwa rubani huyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfalme Abdullah wa Jordan

Imeripotiwa kuwa Jordan imekuwa ikifanya mazungumzo yasoyo rasmi na viongozi wa kikabila katika nchi jirani ya Iraq kuweza kuachiwa huru kwa rabani huyo.