Mwanahabari Greste kurudishwa Australia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Peter Greste kulia na wenzake

Shirika la habari la Misri limesema kuwa mpango wa kumrudisha nyumbani mwanahabari wa shirika la Al jazeera Peter Greste unaendelea.

Duru zinaarifu kuwa baada ya kuhudumia siku 400 akiwa jela,bwana Greste atarudishwa nyumbani Australia.

Yeye na wenzake wawili walipewa kifungo kirefu kwa kushirikiana na kundi la muslim brotherhood lililopigwa marufuku.

Kampeni ya kimataifa ya kutaka watatu hao waachiliwe huru ilianzishwa.

Na mwezi uliopita mahakama ya Misri iliagiza watatu hao kufunguliwa mashtaka upya baada ya kutupilia mbali hukumu ya awali.

Hatahivyo hakuna habari zozote kuhusu hatma ya wenzake Peter Greste.