Wapiganaji wa Alshabaab wauawa Somalia

Image caption Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab

Serikali ya Somalia inasema kuwa takriban wanamgambo 45 wa kundi la Al-Shabab wameuawa kwenye shambulizi la angani.

Gavana wa eneo lililo kusini la Lower Shabelle (Abdulkadir Mohamed Nuur Siiddi) ameiambia BBC kuwa wanamgamnbo kadha wa kigeni ni kati ya wale waliouawa kwenye shambulizi lililoendeshwa kwa ushirikiano kati ya wanajeshi wa Marekani na wale wa muungano wa Afrika.

Alisema kuwa makombora matatu yalishambulia msafara wa Al shaabab na moja katika kambi zake za kutoa mafunzo.