Kaburi la kamanda wa LRA lapatikana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mwanajeshi wa LRA

Jeshi nchini Uganda linasema kuwa limegundua mabaki ya kamanda wa cheo cha juu wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army LRA.

Okot Odhiambo ambaye alikuwa mmoja wa makamanda watano waliokuwa wakitafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huenda aliuawa kwenye mapigano mwaka 2013.

Uchunguzi wa DNA unafanywa kuthibitisha mabaki hayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiongozi wa LRA Jospeh Kony

Kamanda mwingine wa LRA Dominic Ongwen alifikiswa mbele ya mahakama ya ICC wiki iliyopita.

Hata hivyo kiongozi wa LRA Joseph Kony bado yuko mafichoni.