Bobbi Kristina bado yuko hospitalini

Haki miliki ya picha
Image caption Bobbi Kristina akiwa na Mama yake Marehemu Whitney Houston

Wakati Bobbi Kristina akiwa bado Hospitalini, Mwanasheria wa Baba yake amesema kwa sasa wanafanya uchunguzi kubaini kilichomsababishia Bobbi Kristina kulazwa.

Mwanasheria Christopher Brown amesema Mtoto wa waimbaji Marehemu Whitney Houston na Bobby Brown hakuwahi kuolewa na Nick Gordon kama ambavyo ripoti kadhaa zimekuwa zikidai.

Bobbi Kristina Brown alikutwa akiwa amepoteza fahamu akiwa bafuni mwishoni mwa juma. Familia yake imekuwa kimya kuhusu hali yake, lakini Baba yake alitoa taarifa kupitia mwanasheria wake siku ya jumanne.

Bobby Brown ameomba jamii iache ishughulikie mambo ya kifamilia kwa uhuru na kumuonesha upendo bintiye.

Binti huyo alifikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa hakuwa na fahamu hali iliyowafanya kumkimbiza hospitali, mpaka siku ya jumatatu jioni alikuwa bado kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Siku ya jumanne alihamishiwa kwenye Hospitali ya Chuo cha Emory mjini Atlanta, Vyanzo vilivyo karibu na Familia ya Brown vimeeleza.