230 wahukumiwa kifungo cha maisha Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano ya Mwaka 2011 yaliuangusha utawala wa Hosni Mubarak

Mahakama nchini Misri imetoa hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Watu 230 akiwemo mmoja kati ya Wanaharakati vinara walioongoza harakati za kuuangusha utawala wa Hosni Mubarak kwa makosa ya kushiriki katika maandamano dhidi ya Serikali ya Cairo miaka mitatu iliyopita.

Mwanaharakati Ahmed Douma pia ametozwa faii ya Dola milioni 2.2 kwa kosa la kuchoma moto taasisi ya mafunzo ya Sayansi.

Kesi hiyo ilihusishwa na mapigano nje ya majengo ya wizara jijini Cairo mwezi Desemba mwaka 2011.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni pamoja na kuwashambulia Maafisa usalama na kuvamia ndani ya Jengo la Wizara ya mambo ya ndani.

Kwa kosa hilo Douma kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka mitatu.