Kunawa mikono iwe hiari baada ya kutoka mawaliwato

Image caption Kazi ya kunawa mikono iwe hiari binafsi

Seneta mmoja nchini Marekani amewataka wamiliki wa migahawa nchini humo kuacha tabia ya kuwashurtisha wafanyakazi wao kunawa mikono baada ya kutoka maliwatoni.

Seneta Thom Tillis, wa chama cha Republican kutoka North Carolina ,ametoa kauli hiyo mapema wiki hii wakati alipokuwa akipinga kanuni za biashara na kuwataka wafanyakazi waachwe waamue wenyewe kuosha mikono yao, ama lah.

Kauli ya seneta huyo imekuja baada ya kanuni kuelekeza kuwa mgahwa ambao hautawaelekeza wafanyakazi wake kunawa mikono,waache kufanya biashara haraka.

Seneta Tills, akashauri kuwa migahawa ambayo wafanyakazi wake hawanawi mikono wanapaswa kuweka alama wazi kwa wateja wao kama ishara ya utaratibu wao,kauli hii ya pili Tillis aliitoa wakati wa mahojiano na Us Capitol.

Tills akatetea hoja yake kwamba, Kuna wakati zipo kanuni ambazo pengine tunahitaji kuzipa muelekeo,lakini waachi wale ambao wamewekewa kanuni hizo hiyo waamue kama ina leta maana ama lah na wafanye maamuzi hayo kinyume na serikali.

Hoja hii imekuja huku wagombea uraisi walio wengi kutoka katika chama cha Republican,wakiamini kwamba wataulizwa maswali kuhusiana na kanuni na taratibu za chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola

Walau wazazi wawili wao wameonesha msimamo wa dhahiri kuwa wakati mwingine huwataka watoto wao kuikwepa chanjo hiyo pindi wanapohudhuria masomo yao.