Wataalam wa afya kujadili Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maandalizi ya dawa ya ebola nchini Liberia

Kwa upande mwingine madaktari na maafisa wa afya wanakutana mjini London Ijumaa kujadili ni mambo gani ya kuzingatiwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Wajumbe watakuwa wanaangalia uharaka wa kimataifa katika kukabiliana na mlipuko na namna uduni wa miundombinu ya sekta ya afya katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone ilivyosababisha kuenea kwa ugonjwa huu. Wataalam pia watakuwa wanchunguza namna ambavyo dawa mpya za tiba na chanjo ya ugonjwa wa Ebola zinavyofanya kazi.

Alhamisi shirika la utafiti wa tiba la Ufaransa limesema matokeo ya dawa mpya dhidi ya ebola ambazo zinafanyiwa majaribio nchini Guinea zimeonyesha matokeo ya kutia moyo katika kupambana na ugonjwa huo.