Raia wa Jordan waandamana kupinga IS

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Jordan waandamana kupinga islamic state

Maelfu ya riaa wa Jordan wameandamana katika mji mkuu , Amman, wakiunga mkono serikali yao katika vita inavyotekeleza dhidi ya kundi la Islamic State baada ya kumuua rubani wa ndege za vita wa Jordan.

Serikali ya Jordan inasema kuwa ndege zake za vita zilifanya mashambulizi kadhaa ya angani zikilenga wapiganaji wa Islamic State huko Syria Alhamisi.

Maafisa wa usalama wa Jordan wanaarifiwa kuwa ndio waliokuwa wakilengwa na mashambulizi huko Raqqa, eneo lenya ufuasi mkubwa wa IS nchini Syria.

Hadi sasa mataifa manee ya kiarabu yakijumuisha Jordan yanahusika katika kampeni kali inayoongozwa na Marekani dhidi ya Islamic state kupitia mashambulizi ya angani.