Jordan yaapa kuimaliza IS kwa kila hali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfalme Abdullah wa Jordan aahidi kupambana na Waasi wa Islamic State

Jordan imesema mashambulizi ya anga dhidi ya Wanamgambo wa Islamic State ni mwanzo tu wa kulipa kisasi kwa tukio la kumteka nyara Rubani wa nchini humo, Waziri wa mambo ya nje wa Jordan,Nasser Judeh ameeleza.

Judeh ameiambia CNN kuwa Jordan inafanya kila jitihada kupambana na IS.

Awali Jordan ililenga maficho ya wanamgambo nchini Syria, lakini Judeh amesema Operesheni zao zimefika mpaka Iraq.

kauli hii imekuja baada ya Wanamgambo wa IS kuonyesha Video waliokuwa wakimchoma moto Rubani Moaz al-Kasasbeh akiwa hai.

Baada ya shambulio la siku ya Alhamisi,Ndege za kivita zilikwenda mpaka katika Kijiji cha Rubani huyo, ambapo Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili alienda kuonana na Familia ya Marehemu.