Nigeria:Ratiba ya Uchaguzi ni ileile

Haki miliki ya picha
Image caption Uchaguzi wa Nigeria kufanyika Tarehe 14 mwezi huu ilhali hali ya usalama ni tete katika baadhi ya maeneo nchini humo

Nigeria imesema itafanya uchaguzi wa Urais jumamosi ijayo kama ilivyopangwa.Uamuzi huo umekuja baada ya mkutano uliofanyika kwa saa saba mjini Abuja kati ya Wagombea, Magavana wa Majimbo na Tume ya uchaguzi.

Hakuna kituo chochote cha kupiga kura kitakachokuwepo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambapo Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wamekuwa wakidhibiti.

Watu waliokimbia mapigano watapata fursa ya kupiga kura katika maeneo mengine,ingawa bado taarifa za kina zinatakiwa kutolewa.

Baadhi ya majimbo yametangaza siku za mapumziko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Watu wanapata nafasi ya kuhakikisha kuwa wako katika orodha ya wapiga kura.