Waasi wa Houthi wachukua serikali Yemen

Image caption Waasi wa Houthi wachukua uongozi Yemen

Waasi wa Shia wametangaza kutwaa uongozi wa kisiasa nchini Yemen, kuvunjilia mbali bunge, kumwondoa rais na nafasi hiyo kuchukuliwa na baraza la urais.

Wahouthi hao walitangaza hayo katika mkutano wa siasa walipokuwa najeshi na wakuu wa makabila katika ikulu ya nchi katika mji mkuu, Sanaa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi wa Houthi

Tukio hilo linajiri baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na umoja wa mataifa ya kukomesha mzozo wa Yemen kusambaratika.

Rais Mansour Abdrabbuh Hadi na serikali yake walijiuzulu mwezi uliopita baada ya waasi hao kuthibiti mji wa Sanaa.