Aganda katika barafu akimtafuta mpenziwe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Barafu kali

Raia mmoja wa Uturuki aliganda na kuwa barafu baada ya kujaribu kuingia ndani ya ndege ili kwenda kumuona mpenziwe nchini Uingereza.

Hikmet Komur mwenye umri wa miaka 32 alitamani sana kumuona mpenziwe Luisa da Silva swala lililomlazimu kupanda katika gea ya kutua kwa ndege moja ya Uingereza nchini Istanbul.

Lakini alifariki alipokuwa katika safari kutokana na baridi kali ya vipimo vya chini vya -60c ambayo ilimuathiri ubongo wake.

Kabla ya safiri alimwambie mwanawe kwamba atasafiri kwa siku chache.

Mwili wa bwana Komurs ulipatikana katika uwanja wa ndege wa Heathrow baada ya wafanyikazi katika uwanja huo kuona miguu ya binadamu.