Bomu lalipuka nje ya ikulu ya rais Yemen

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ikulu ya rais nchini Yemen

Bomu limelipuka nje ya ikulu ya rais wa Yemen, katika mji mkuu, Sanaa, mji ambao sasa unadhibitiwa na wapiganaji wa madhehubu ya Shia, wa Houthi

Inaarifiwa kuwa waasi wawili wa Houthi walijeruhiwa.

Hapo jana wapiganaji hao walilivunja bunge kabla ya kudhibiti madaraka.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wapiganaji wa Houthi

Sasa wapiganaji hao wamebuni halmashauri ya usalama kuongoza nchi hadi bunge la muda litakapoundwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua zaidi, iwapo wapiganaji hao hawatarudi haraka kwenye mazungumzo, kuhusu kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye demokrasi.

Baraza jiiya limewataka wapiganaji wamuachilie huru rais wa Yemen, waziri mkuu, na baraza la mawaziri kutoka kifungo cha nyumbani.