Mbunge auawa nchini Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari la mbunge aliyepigwa risasi nchini Somalia.Mbunge mwengine nchini Kenya amepigwa risasi na kuuawa ndani ya gari lake

Mbunge mmoja ameuawa kwa kupigwa risisi kwenye mji mkuu wa kenya Nairobi.

Ripoti za polisi zinasema kuwa mbunge huyo wa Kabete, eneo lililo nje kidogo ya mji wa Nairobi aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Walinzi wake wawili,dereva pia nao wameuawa.

Polisi wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha walilifuata gari la mbunge huyo kutoka eneo la Westlands kabla ya kulimiminia rasasi ndani ya mji wa Nairobi.