Wakilii azua mjadala kuhusu ubakaji UK

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mahakamani

Wakili mmoja nchini Uingereza amezua mjadala baada ya kusema kuwa wanaume hawafai kushtakiwa na ubakaji iwapo mwanamke aliyetendewa uovu huo amelewa pombe ama anatumia dawa za kulevya.

David Osborne alitoa madai hayo katika blogu ya mtandao wake aliouita ''She was gagging for it''.

Matamshi yake yalisababishwa na Alison Saunders,mkurugenzi wa mashtaka aliyetangaza kwamba mikakati itawekwa kubaini iwapo mwanamke yuko katika hali nzuri kutoa ruhusa.

Osbone mwenye miaka 71 aliandika:''Katika kitabu changu ruhusa ni ruhusa ,uwe kipofu,mlevi ama hali yoyote ile.

Majuto baada ya kitendo hicho hayawezi kubadilisha hali na kusema mtu amebakwa.Nina suluhu rahisi ambayo nadhani mutaikubali.

''Iwapo mlalamishi alikuwa chini ya shinikizo la pombe ama dawa za kulevya wakati alipobakwa hii inampa mshtakiwa ngao katika kesi inayomkabili.

Je, unakubaliana na matamshi ya wakili huyu?kwa maoni yako basi ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili.