Fainali:Ghana kumenyana na Ivory Coast

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Asamoah Gyan kukiongoza kikosi chke katika mechi ya leo

Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan huenda atashiriki katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast baada ya kupata nafuu ya jeraha la kiuno.

Mshambuliaji huyo alipata jeraha hilo baada ya kugongana na kipa wa Guinea Naby Yattara katika robo fainali na aliorodheshwa miongoni mwa wachezaji wa ziada wakati kikosi cha Ghana kilipocheza katika mechi ya nusu fainali.

Haki miliki ya picha afp
Image caption Yaya Toure kukiongoza kikosi ch Ivory Coast

Vilevile Ivory Coast itamkosa kiungo wake wa kati Cheick Tiote ambaye hajapona jeraha la mguu.

Miamba hiyo ya ''The elephants'' itategemea mchezo mzuri kutoka kwa nahodha wao Yaya Toure kuilaza Ghana.