UN yataka rais wa Yemen arudi mamlakani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ban Ki Moon ataka rais wa zamani wa Yemen kurudi mamlakani

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa rais wa zamani wa Yemen, Abedrabbo Mansour Hadi, lazima arejeshwe madarakani.

Rais na serikali yake walijiuzulu mwezi uliopita, baada ya wapiganaji wa Houthi, kudhibiti mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Bwana Ban Ki-moon alisema hali sasa ni ngumu, ngumu sana, na kusema kuwa Houthi wamesababisha utupu kwenye uongozi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Yemen aliyejiuzulu Abedrabbo Mansour Hadi

(Mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu, Nabil Al Arabi alishtumu unyakuzi huo wa mamlaka akionya kuwa utaangusha mfumo wa demokrasi nchini humo.

Siku ya jumamosi maelfu ya raia wa Yemen walifanya maandamano katika miji kadhaa katikati ya taifa hilo wakipinga unyakuzi huo wa mamlaka.